Home KITAIFA PUMA ENERGY YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 12.2, RAIS DK. SAMIA APONGEZA

PUMA ENERGY YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 12.2, RAIS DK. SAMIA APONGEZA

Dar es Salaam

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imepongezwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira Mazuri ya uwekezaji ambayo yamesababisha kuweza kukabidhi gawio la Sh.Bilioni 12.2 kwa Serikali na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zao ili kufanya vizuri zaidi.

Gawio hilo wamelikabidhi leo Juni 11,2024  Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dk. Samia ambapo pia ameweza kupokea gawio kutoka kwa Kampuni 10 ambazo Serikali inahisa zake na Kampuni ya  Kampuni ni miongoni mwake.

Akizungumza baada ya kukabidhi gawio, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah amesema wanamshukuru Rais Dk. Samia ambaye ndio jemedari wetu wa  kiuchumi nchini Tanzania.

”  Rais Dkt Samia ameweza kutoongoza vizuri, ameweka mazingira wezeshi kwa sisi wawekezaji kufanya biashara kwa usalama na ubunifu .Pia tunatoa shukrani kwa Wizara ya Nishati chini ya  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko wamekuwa ni viongozi ambao  wanatuelekeza na kutushauri lakini wamekuwa wakiweka mazingira yanayotuwezesha kufanya kazi vizuri .

“Pia tunamshukuru Msajili wa Hazina ambaye amekuwa kiungo muhimu kwetu sisi kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri na  hatimaye tumetoa gawio leo la  shilingi bilioni 12.2 .Kigezo  kikubwa ambacho kimewazesha kutoa gawio hilo kinatokana na kufanya kazi vizuri Bodi yetu chini ya Mwenyekiti Dk . Selemani Majige ambao wamekuwa wakituelekeza na kutupa ushauri mzuri,”amesema Fatma.

Amefafanua zaidi kuwa katika kuendeleza ufanisi kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma na kuziboresha na kwamba mikakati yao ni kutoa huduma kidigitali na  katika kutoa huduma zao  mwaka huu wamepanga kuwafikia watanzania wengi kwenye kusambaza nishati.

Pia amesema wameona Serikali ilivyoweka nguvu katika nishati safi hivyo na wao wameamua kuweka nguvu katika kufanikisha malengo ya serikali katika eneo la Nishati Safi ya kupikia kama ilivyo dhamira ya Rais Dk Samia ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi.

Ameongeza kuwa wana mpango wa kuzindua kituo cha gesi kwa ajilli ya kujaza katika magari na uzinduzi huo wanatarajia kuufanya mwaka huu huku akisisitiza wanajivunia kutoa gawio hilo kwani kumekuwa na ongezeko kubwa kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here