Home KITAIFA WAHANDISI WASHAURI NCHINI WATAKIWA KUSIMAMIA KWA UKARIBU UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA

WAHANDISI WASHAURI NCHINI WATAKIWA KUSIMAMIA KWA UKARIBU UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Tabora

NAIBU Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu OR-TAMISEMI Mhandisi Rogatus Matavila amewataka Wahandisi Washauri wanaosimamia miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara nchini kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Mhandisi Matavila ameyasema hayo leo Juni 10 2024 wakati akikagua ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi katika manispaa ya Tabora ambalo lipo chini ya mradi wa TACTIC unaosimamiwa na TARURA.

” Rais Dk. samia Suluhu Hassan anahangaika kutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wanapata barabara,wataalam lazima mbadilike na kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi hii.
Mkandarasi huyu angekuwa anasimamiwa kwa ukaribu angeshakuwa amemaliza hapa,”amesema.

Mhandisi Matavila amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa ujenzi ili wakandarasi wakamilishe kazi kwa wakati.

Aidha, amemtaka Mhandisi Mshauri UNITEC Civil Consultants ltd kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi huo na ifikapo mwezi Agosti mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika.

Ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi linalogharimu takriban milioni 800 lilianza ujenzi wake Novemba 2023 na lilitarajiwa kukamilika Juni, 15 2023 na kuagiza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Agosti 2024 na linajengwa na mkandarasi CICO Contractor.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here