Home KITAIFA TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI- DK. BITEKO

TANZANIA INA UMEME WA KUTOSHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI- DK. BITEKO

📌 Asisitiza hakuna mgawo wa umeme

📌 Amshukuru Rais Samia kuiimarisha Sekta ya Nishati

Geita

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema kuwa, kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha kuwawezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Dk. Biteko amesema hayo leo Juni 9, 2024 wakati alipoungana na Waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwenye ibada ya jumapili.

“Nashukuru Rais, Dk. Samia ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imepelekea tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme,” amesema Dk. Biteko.

Ameongeza kuwa, miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme lilikuwa likimkosesha amani, lakini kwa juhudi za viongozi Wakuu wa Serikali, Wizara na TANESCO limefikia tamati.

Kutokana na uwepo wa umeme mwingi wa kutosha, Dk. Biteko amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here