Home KITAIFA SMART DARASA YAWAFUNGULIA MILANGO WADAU WAPYA WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO...

SMART DARASA YAWAFUNGULIA MILANGO WADAU WAPYA WA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO KATIKA ELIMU

Na Mwandishi wetu

WADAU wa Elimu nchini waaswa kutumia ubunifu mbalimbali kuhakikisha wanaongeza ufaulu na Kurahisisha nyezo za Watoto Mashuleni Kujifunza kwa Kutumia mifumo ya Teknolojia.

Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi wa Utafiti Habari katika Machapisho ya Elimu Nchini(TIE) Kwangu Zabron mara baada ya Kutambulishwa kwa program mpya Kusaidia Matumizi ya Teknolojia,Mawasiliano na Habari katika Elimu (SMART DARASA) amesema uwepo wa Wadau wa Elimu wengi unaleta mchango mkubwa kwa Serikali hasa katika mlengo wa kuboresha Elimu nchini.

“Kama tunavyofaham kupitia maelekezo na Maagizo kutoka kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alielekeza kuboresha Mitaala ambayo inalenga kujenga ujuzi,ambapo mitaala hiyo iliyoboreshwa mwaka 2023 ambayo imeanza kutumika kwa shule za awali pamoja na Kidato cha tano imezingatia zaidi ujenzi wa umahiri ikiwemo matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),”amesema

Ameongeza kuwa kupitia mtaala huo ulioboreshwa mtaala huo unaruhusu mtoto kuanzia ngazi ya Elimu ya awali kuanzia kujifunza tehama katika nafasi yake (LEVEL) .

Pia amesema Matumizi hayo ya Tehama Yana nafasi kubwa kwa watoto kwa kuboresha Elimu katika Nyanja zote.

“Kuwepo kwa Wadau wa Elimu hawa (SMART DARASA) ni Maono sahihi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Maono sahihi ya Wizara ya Elimu Kuwaleta karibu Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kujifunza na ufundishaji kutokana na Maudhui ya mfumo wa wadau hao ulivoandaliwa ambapo itamuwezesha Mwalimu kufundisha mada ngumu na kumrahisishia Mwanafunzi kufanya Mazoezi kivitendo na nadharia,”amesema.

Pia ametoa wito kwa wadau wa Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni wakati muafaka na mitaala inaruhusu na Serikali inakaribisha Wadau Mbalimbali waje kufanya Kazi pamoja na serikali lengo likiwa kuisadia Elimu ya Tanzania,Kumsaidia Mtoto wa Tanzania ili anapokuwa amehitimia masomo yake aweze kufanya na kutenda vitu vikatokea kwa ufanisi.

Kwa upande wake Meneja Biashara na Tehama (SMART DARASA) Faith Silaa amesema program hiyo imeambatana na akili bandia (ARTIFICIAL INTELLIGENCE) ambapo imekuwa ikiongelewa sana na kutumika hivyo kama (SMART DARASA ) wanaitumia kumuwezesha Mwanafunzi kufanya Majaribio anayokutana nayo bila kukariri na itamuwezesha kufanya Majaribio hayo hatua kwa hatua.

Amesema utofauti wa program hiyo unaweza kuperuzi bila bando kutokana na uwezo wa kuzipakuwa mifumo mbalimbali na program hiyo.

“Tumetambulisha program mpya inayolenga Kusaidia watoto kujifunza ki nadharia na kujenga uwelewa katika masomo kwa njia ya Tehama (SMART DARASA),”amesema.

Aidha Program hiyo inatarajiwa kuanza rasmi Julai 1,2024 ambapo itawawezesha na itasaidia kwa kiasi kikubwa ufaulu wa Wanafunzi nchini.

Pia amesema Mikakati yao ni kuwafikia Wanafunzi na Kuwaelekeza na namna ya kuitumia pamoja na kutembelea shule mbalimbali na kuzungumza nao faida ya program hii ya smart darasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here