Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA 23 WA WAKUU WA NCHI

RAIS DK.SAMIA ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA 23 WA WAKUU WA NCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini mazungumzo wakati aliposhiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam Juni, 7 2024. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa EAC Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit. Viongozi wengine walioshiriki katika Mkutano huo ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Somalia Dk. Hassan Sheikh Mohamud, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi na Makamu wa Rais wa Burundi Prosper Bazombanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akichangia majadiliano wakati aliposhiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam Juni, 7 2024. Mkutano huo umempitisha Veronica Mueni Nduva (Raia wa Kenya) kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. Nduva ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa EAC. Marais hao wamekubaliana kufanyike Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Mtangamano kujadili masuala ya amani, ulinzi na usalama pamoja na changamoto zingine zinazoikabili EAC ili kuwasilisha ripoti hiyo kwenye Kikao kijacho cha Wakuu wa Nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here