Home KITAIFA MUWASA YAENDELEA KUSAMBAZA MAJI YA BOMBA KWENYE KATA 4 MUSOMA VIJIJINI

MUWASA YAENDELEA KUSAMBAZA MAJI YA BOMBA KWENYE KATA 4 MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma ( MUWASA) imeendelea na zoezi la usambazaji maji ya bomba kwenye Kata 4 jimbo la Musoma vijijini.

Kata ambazo zoezi hilo linafanyika ni Etaro,Nyegina,Nyakatende pamoja Ifulifu ambazo zote zinaendelea kufikishiwa vifaa yamefikishwa kwenye kata ya Nyigine kwaajili ya kusambazwa kwa wananchi.

Akizungumza leo Juni 5 juu ya zoezi la usambazaji wa mabomba hayo,Kaimu Meneja Uhusiano wa (MUWASA) Chiku Joseph amesema zoezi usambazaji unaendelea vizuri kwa kufikisha maeneo yote yanayo husika.

Amesema wakati mabomba hayo yakifikishwa maeneo husika wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kulinda miundombinu hiyo.

Chiku amesema MUWASA imepewa jukumu la kufikisha huduma ya maji maeneo hayo na itatekeleza ili wananchi waweze kupata maji.

” Tunaendelea na usambazaji wa mabomba kwenye Kata hizo 4 na leo tumefikisha kwenye Kata ya Nyegina ili kuwafikishia huduma wananchi wa Musoma vijijini,”amesema

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uamuzi wa serikali wa kusambaza maji ya bomba kwenda kwenye kata hizo nne kutoka chanzo cha maji ya Musoma mjini kilichopo Bukanga itafikisha maji kwa wakati.

Amesema vilevile baadhi ya kata hizo zitasambaziwa maji ya bomba kutoka kwenye bomba kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama huku Kijiji cha Nyasaungu Kata ya Ifulifu kimeanza kutumia maji ya bomba kutoka Mugango.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here