Dodoma
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Suzan Kunambi (MNEC) amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa N Jokate Mwegelo (MNEC) aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ambae kwa sasa ni Katibu Mkuu wa UVCCM.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi Juni 4, 2024 katika Ofisi za Makao Makuu ya UWT jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya Makabidhiano hayo Katibu Mkuu Kunambi amesema ataendeleza na kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake (Jokate) huku akiongeza kasi ya utendaji wa kazi utakaoimarisha jumuiya ya UWT ikiwemo kuvumbua fursa kwa wanawake,kuimarisha Siasa na kukuza Uchumi wa Jumuiya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu. Jokate amempongeza Katibu Mkuu Kunambi kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo na kumtakia kheri ya utumishi na utendaji ndani ya Jumuiya na Chama.