Home AFYA WAUGUZI WANAOHUDUMIA WATOTO WENYE SARATANI WAJENGEWA UWEZO MUHIMBILI

WAUGUZI WANAOHUDUMIA WATOTO WENYE SARATANI WAJENGEWA UWEZO MUHIMBILI

Dar es Salaam

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Taasisi ya Global Hope pamoja na Tumaini la Maisha wameendesha mafunzo kwa wauguzi yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kuwahudumia watoto wenye saratani wanaohudumiwa hospitalini hapa.


 Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga MNH, Redemptha Matindi hospitali ina Kitengo kikubwa cha kuhudumia watoto wenye saratani kutoka sehemu mbalimbali nchini chenye vitanda 78 hivyo mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa watoa huduma.
 
Redemptha amesema kuwa ushirikiano ulipo baina ya MNH, Global Hope na Tumaini la Maisha ulianza tangu mwaka 2018 ambapo umekuwa na manufaa makubwa kwani wamekuwa kuendesha mafunzo kwa wauguzi pamoja na kusaidia katika upatikanaji wa baadhi ya dawa za saratani.

“Napenda kuchukua fursa hii kupongeza juhudi zinazofanywa na Global Hope na Tumaini la Maisha katika kusaidia kuboresha huduma za watoto wenye saratani hapa MNH  hivyo mafunzo haya yaende sambambama na uboreshaji wa huduma za uchunguzi, tiba na utafiti kwani  Serikali pekee haiwezi kumudu mahitaji yaliyopo ya kuongeza idadi ya wataalam wenye ujuzi, kusaidia watu kupata uchunguzi, matibabu na matunzo ya watoto wenye saratani nchini,” amesema Redemtha.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Juni 3 hadi 4 2024 na yamehusisha wauguzi kutoka MNH pamoja na Hospitali ya Jeshi Lugalo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here