Home KIMATAIFA RAIS DK.SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA POSCO

RAIS DK.SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA POSCO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MhSamia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya POSCO International pamoja na viongozi wao Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea Juni, 3 2024. Kampuni hiyo imewekeza katika uchimbaji wa Madini ya Kinywe katika Mgodi wa Mahenge Graphite ambao ni mradi mkubwa wa pili Kidunia wa Madini hayo. Ujumbe huo Umeongozwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Ghang In-Hwa, Rais wa POSCO Kye-in Lee pamoja na Wajumbe wengine wa Kampuni hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya POSCO International inayowekeza kwenye Uchimbaji wa Mradi wa Madini wa Mgodi wa Mahenge Graphite ambao ni mradi mkubwa wa pili Kidunia wa Madini hayo. Ujumbe huo Umeongozwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Ghang In-Hwa. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Seoul Jamhuri ya Korea Juni 3 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here