Dar es Salaam
MTIANIA wa nafasi ya Urais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Barnabas Samwel amesema kumekuwa na changamoto kutoka kwa baadhi ya watu kwa manufaa yao binafsi na familia zao kuingiza siasa katika maslahi ya wanafunzi.
Akizungumza leo Juni 3 jijini Dar es Salaam Mtiania wa nafasi ya urais IFM Barbabas amesema serikali kufuata Sheria na kanuni zinazozuia wanafunzi kujihusisha na masuala ya siasa.
“Kwa bahati mbaya kumekuwa na baadhi ya watu kukandamiza wanafunzi wamekua wakileta ukandamizaji na skendo mbalimbali za kwamba huyu kuna maelekezo kutoka juu basi atakatwa mimi kinachonishangaza ni kwamba je kunakua na maelekezo gani tena kutoka juu na hayo maelekezo yanatoka wapi na wakati Katiba TCU Regulations Act na IFMSO Constitution inakataa yoyote kujihusisha na masuala ya siasa,” amesema Barbabas.
Aidha amesema atasaidia kuondoa dhana kandamizi iliyojengeka kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopewa haki moja ya kupiga kura kwa viongozi wa juu kwa kutogombea nafasi za uongozi kuwa na sifa ya kugombea na kupigiwa kura za nafasi za juu ikiwemo Urais.
Mbali na Barnaba anayetaka nafasi ya Urais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho amembatana na Mike Diakite ambaye ni Mtiania mweza wa nafasi ya U urais katika kurudisha fomu ya nafasi hiyo ambapo uchaguzi unatarajia kufanyika Juni mwaka huu.