Na Shomari Binda-Musoma
DIWANI wa viti maalum manispaa ya Musoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji Amina Masissa amehimiza jamii kuwa na utaratibu wa kufanya usafi kwenye maeneo yao majumbani na kwenye biashara.
Kàuli hiyo ameito hii leo juni 3 wakati wa shughuli ya usafi maeneo ya soko la Nyasho na stend ikiwa ni moja ya matukio ya wiki ya mazingira.
Eneo likiwa safi nyumbani au eneo la biashara licha ya kiafya lakini pia uvutia kimazingira
Amesema suala la usafi sio kusubili wakati wa matukio bali kila wakati mazingira yapaswa kuwa safi kwani yapo magonjwa yanayosababishwa na uchafu.
Diwani Amina amesema eneo la biashara likiwa safi linawavutia wateja na kujiongezea kipato na kuhimiza kuzingatia usafi
” Leo tunashiriki usafi wa mazingira kwenye eneo hili la Nyasho sokoni na stend lakini kila moja anapaswa kufanya usafi majumbani na kwenye maeneo ya biashara.
” Usafi usisubili matukio kama haya ya wiki ya mazingira bali wakati wote uwe wa usafi kwenye majumba yetu na maeneo ya biashara”,amesema Amina.
Amesema katika muendelezo wa matukio ya wiki ya mazingira kesho juni 4 watapanda miti kwenye chuo cha maendeleo ya jamii Buhare na kushiriki kongamano la kimazingira.