Home BIASHARA BRELA YATOA ELIMU MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII TANGA.

BRELA YATOA ELIMU MAONYESHO YA BIASHARA NA UTALII TANGA.

Na Boniface Gideon,Tanga

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wameendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara na Wananchi pamoja na kufanya huduma mbalimbali za kusajiri Makampuni, kusajiri majina ya alama za Biashara, kusajili Leseni za Biashara , kutoa Leseni za viwanda pamoja na hataza,


Elimu hiyo na utoaji wa huduma hizo unafanyika katika maonesho ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.

Afisa Usajili kutoka BRELA Julieth Kiwelu amewaeleza Waandishi wa Habari mapema leo kuwa, huduma zote ambazo hutolewa ofisini kwao kwasasa zinatolewa kwenye maonyesho hayo.

“Huduma zote zinazotolewa ofisini kwetu kwasasa zinapatikana kwenye maonyesho haya ya Biashara na Utalii,hivyo tunawaomba Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali waje hapa wapate huduma zote ambazo hutolewa ofisini kwetu,” ameongeza Julieth

“Kazi kubwa ya maonesho haya ni kutoa Elimu na huduma kwaufumbuzi na alama za Biashara na huduma,kwetu sisi tumeichukulia hii kama fursa ya kutoa Elimu,na tukumbuke kuwa sehemu ya Elimu hii ni uvumbuzi,na sisi BRELA uvumbuzi ndio kazi kubwa tunayoifanya ,wengi hawafahamu nini cha kufanya baada ya kuvumbua kitu , kwahiyo tunachokifanya nikuwapatia Elimu sahihi nini chakufanya baada ya kuvumbua,”amesema Julieth

Amesema wataendelea kutoa Elimu juu Usajili wa Biashara na Leseni nakuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanasajili huduma mbalimbali wanazozitoa.

“Tunawaomba wadau wetu wasajiri huduma wanazozitoa ili ziwe na vibali ,na sisi tupo tayari wakati wowote kutoa huduma,na tutaendelea kushirikiana na Wadau wetu na wasichoke kutuuliza pale wanaposhindwa kutimiza vigezo,” ameongeza

Amesema kwasasa kusajili Biashara na kupata Leseni za ‘BRELA’ ni rahisi na wanaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao.

“Unaweza kupata huduma kwa njia ya mtandao na ukapata huduma ,pia tunawaomba wavumbuzi waje kwetu ,waache kusikiliza maneno ya mtaani mana watapotoshwa na watapata Elimu isiyo sahihi,” amesema Julieth

            

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here