DODOMA
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga ameishukuru Serikali ya marekani kupitia ubalozi wake hapa nchini kwa kudhamini kituo cha kisasa cha Tehama katika Maktaba ya Dodoma kitakachotumika na watanzania kupata maarifa na stadi mbalimbali zitakazo wawezesha kutimiza ndoto zao
Ametoa shukrani hizo mei, 30 2024 Jijini dodoma alipohudhuria ufunguzi wa Maktaba hiyo ya kisasa iliyodhaminiwa na Serikali ya marekani na kutoa rai kwa watanzania kutumia Maktaba hiyo
Kipanga ameingeza kuwa maktaba hiyo pamoja na uwepo wa vitabu pia imeunganishwa na mkongo wa taifa ili kuwezesha upatikanaji wa vitabu na maharishi mbalimbali kwa njia ya mtandao.
Pia ameitaka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kukitunza kituo na hicho na vifaa ili vidumu kwa muda mrefu na kuwanufaisha watanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Michael Battle emesema wataendelea kuwekeza katika kuanzisha vituo vya aina hiyo katika maktaba sehemu mbalimbali nchini ili kutoa fursa ya kuongeza maarifa kwa vijana wa kitanzania ili waweze kutumiza ndoto zao na kuwa na uelewa mkubwa juu ya teknolojia mbalimbali zinazotumika ulimwenguni.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Hudumu za Maktaba nchini Dk. Mboni Ruzegea amewakaribisha watanzania kutumia Maktaba hiyo ya kisasa kujipatia maarifa na taarifa mbalimbali zitakazo wasaidia kwenye masomo tafuti na kuongeza maarifa bila gharama yoyote.