Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili iko kwenye hatua mbalimbali za kutumia mifumo ya kidigitali katika baadhi ya maeneo ya kutolea huduma ili kuongeza ufanisi na kuboresha utendaji kazi.
Akizungumza leo Mei 30 na baadhi ya viongozi kutoka katika kampuni ya GE Healthcare na Computech zinazohusika na kufunga mifumo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Profesa Mohamed Janabi amesema kuwa mifumo hiyo itafungwa vyumba vya upasuaji, vyumba vya kujifungua pamoja na vyumba wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).
“Hii ni hospitali ya taifa na ndio hospitali inayohudumia wagonjwa takribani 4000 kwa siku hivyo ni wakati sasa wa kutafuta mifumo kama hii ambayo itasaidia kuboresha huduma na kurahisisha utendaji kazi haspitalini hapa,”amesema Profesa Janabi.
Kwa upande wake Msimamizi wa Suluhisho la Mambo ya Mifumo ya Kidigitali kwa Wagonjwa kutoka Computech, Walid Fayad amesema mifumo hiyo itafungwa katika baadhi ya vifaa vinavyotumika katika maeneo ya kutolea huduma na ili kusaidia kujua kama kifaa kimetumika muda gani na nani anakitumia, kimetumia vitendanishi kiasi gani n.k.
Ameongeza kuwa mifumo hiyo pia inaweza kubaini kama mgonjwa alishafanyiwa kipimo fulani na endapo atafanyiwa kipimo ambacho alichawahi kufanyiwa kabla mifumo hiyo itaweza kulinganisha majibu ya kipimo anachofanyiwa siku hiyo na wakati uliopita