Home KITAIFA SERIKALI IPO TAYARI KUTOA FEDHA KUREJERESHA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA NA MVUA

SERIKALI IPO TAYARI KUTOA FEDHA KUREJERESHA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA NA MVUA

Na Esther Mnyika@Lajiji Digital 

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandisi Rogatus Mativila amesema wameshafanya tathimini  ya kurejeresha miundombinu iliyoharibiwa na mvua zinahitaji  kiasi cha shilingi bilioni 2 na Serikali ipo tayari kutoa fedha hizo.

Pia teknolojia mbadala kuimarisha mtandao wa barabara ikiwemo ujenzi wa madaraja imara na madhubuti itaendelea kutumiwa nchini na Wakala ya Barabara za Vijijini na Vijijini  (TARURA) .

Hayo ameyabainisha Mei 27 na Mhandisi Mativila alipotembelea  banda la TARURA liliopo kwenye maonesho  ya Mkutano wa 30 wa Kimataifa wa Wahandisi Washauri Afrika unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam.

“Miundombinu iliyoharibiwa na mvua zilizoanza kunyesha tangu Oktoba mwaka jana barabara zimeharibika zinapitika kwa shida ambazo zinakuwa zimekatika hakuna  mawasiliano  kati ya sehemu  moja hadi  nyingine  hivyo huwezi kurekebisha barabara mvua zinaendelea kunyesha, “amesema. 

Ameeleza kuwa Ili waweze kufanya marekebisho lazima  mvua ziwe zimeisha kuhakikisha mawasiliano yanarudi wanatarajia kuanzia Julai  mwaka huu maji yatakuwa yamekauka kujenga  wakati kama kuna maji au mvua watakuwa wanapoteza fedha za wananchi. 

Amesema TARURA wanaonesha utaalamu wanafanya ikiwemo ujenzi wa ‘structure’ mbalimbali za kupitishia maji, wanajenga kwa mawe teknolojia ambayo inapunguza gharama.

Mhandisi Mativila  amesema vitu ambavyo  vinaoneshwa  hapo ni teknolojia  nyingine za  kutumia  kemikali na malighafi zingine katika kuhakikisha  malighafi zilipo maeneo  hayo kwa mfano barabara  ina udongo  wa mfinyanzi  inaweza kutumia  kemikali  fulani ikabadilika  ikawa imara  na kujenga  barabara kwa gharama nafuu. 

Kwa upande wake Msimamizi wa Teknolojia Mbadala TARURA – Makao Makuu Mhandisi Mshauri Pharels Ngeleja amesema tayari wamejenga madaraja 256 kwa teknolojia ya mawe yaliyogharimu shilingi Bilioni 13.

“Teknolojia ya mawe tunatumia pia kujenga barabara, kuna Kilometa. 26.18 zimekamilika Mkoani Mwanza, Kigoma na Rukwa, pia kwenye barabara zetu zingine tunatumia teknolojia za Ecoroad, Ecozyme na Polymer,”amesema 

Ameongeza kuwa wamejenga barabara ya Sawala Kilometa 13 Mkoani Iringa, Chamwino – Dodoma pia wanaendelea na hizo teknolojia, Dodoma kuna barabara inaitwa daraja dogo wamekamilisha miradi hiyo ipo maeneo mbalimbali.

Vilevile amesema TARURA kupitia kitengo cha mambo ya mazingira wanaendelea pia kufuatilia kwa ukaribu athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kujiimarisha zaidi katika ujenzi wa miundombinu yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here