Home AFYA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE YENYE THAMANI YA MILIONI 16.9.

MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE YENYE THAMANI YA MILIONI 16.9.

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine POCUS yenye thamani ya shilingi miloni 16.9 kutoka kwa wafadhili wa mradi wa Himofilia (Novo Nordisk Foundation na Novo Nordisk Haemophilia Foundation) ambayo itahudumia wagonjwa wenye magonjwa ya damu (HIMOFILIA).
 
Akipokea msaada huo Mei 28 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MNH, Dk. John Rwegasha amesema mashine hiyo itatumika katika kufanya uchunguzi na kufuatilia maendeleo ya ugonjwa katika maungio ya wagonjwa na kusaidia kupunguza matumizi ya dawa yasiyokuwa ya lazima kwa wagonjwa wa Himofilia kwakuwa sio kila maumivu aliyonayo mgonjwa yanayosababisha na kuvuja damu.

Amesema mashine hiyo itawezesha mtalaam kuona kama mgonjwa amevuja damu sehemu za ndani mathalani kwenye goti, tumboni au misuli kwa urahisi na haraka ambapo ingekuwa ngumu kutambua kwa macho.
 
Ameongeza kuwa pamoja na kutoa msaada wafadhili hao pia wataendesha mafunzo ya siku nne ambapo yataanza Mei 28 hadi 31 M2024 ambapo yatatolewa kwa wataalam wa Utengamao.

“Ninawashukuru Wafadhili wetu Novo Nordisk Foundation na Novo Nordisk Haemophilia Foundation kwa uwezeshaji wao kwani pamoja na kutupatia msaada pia wametuletea mtaalam aliyebobea zaidi katika mashine hiyo ya POCUS kutoka nchini Kenya ambaye atawejengea uwezo wataalam wetu namna nzuri ya kutumia mshine hiyo,” amesema Dk. Rwegasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here