Home KITAIFA DK.MPANGO ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

DK.MPANGO ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuzindua Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya Mwaka 2024 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2024 jijini Dodoma.

Akizungumza Mei 27, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk. Selemani Jafo amesema miongozo hii imelenga kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika rasilimali za uchumi wa buluu.

Amefafanua kuwa Makamu wa Rais pia atagawa vyeti vya kutambua kampuni zilizoidhinishwa kuanza utekelezaji wa miradi ya kaboni pamoja na kukabidhi hundi kwa Halmashauri ya Katavi pamoja na kutambua mchango wadau katika kushiriki utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.

“Katika wiki hiyo ya mazingira, pia kutakuwa na Kongamano la Kitaifa la wadau wa Mazingira ambalo litakuwa na kaulimbiu isemayo “Mabadiliko ya Tabianchi na Athari zake” litakalofanyika Mei 31, 2024 jijini Dar es Salaam,”amesema.

Amesema kongamano hilo ambalo mgeni Makamu wa Rais limeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), litafanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Pia katika kuchaguza wiki ya mazingira, Dk. Jafo amesema anatarajiwa kuzindua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa chini ya Mradi wa Urejeshaji wa Uoto wa Asili unaotekelezwa katika mikao mbalimbali nchini mikoa hiyo ni Mkoa wa Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi Mei 29, 2024.

Vilevile amesema kutakuwa na Maonesho ya Wiki wa Mazingira ambapo wadau mbalimbali watapata fursa ya kuonesha bidhaa, teknolojia, uvumbuzi na ubunifu wa masuala mbalimbali yanayohusu hifadhi na uzimamizi wa mazingira.

Maonesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma na kuzinduliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko.

Dk. Jafo ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika kuadhimisha maadhimisho haya kwa kushirikiana na Serikali katika shughuli hizi za maadhimisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here