Home KITAIFA WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA...

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA BRAZIL

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Tax Mei, 17 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Brazil, Jenerali Rodriques Heraldo Luiz, mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yalilenga kuimarisha ushirikiano baina na ya Tanzania na Brazil katika Diplomasia ya Ulinzi.

Katika kikao hicho, Waziri Tax amemhakikishia Jenerali Rodriques Heraldo Luiz, utayari wa Tanzania kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT kushirikiana na nchi ya Brazil katika nyanja mbalimbali za Ulinzi hususan katika ubadilishanaji wa wataalamu, Mafunzo pamoja na ushirikiano dhidi ya changamoto za kiusalama kama uhalifu wa mtandaoni na vita dhidi ya ugaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here