Na Mwandishi wetu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi .Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inathamini sana mchango wa Benki ya CRDB katika kukuza uchumi wa Zanzibar na kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar
Pia ameeleza kuwa CRDB imechangia kuendeleza sekta mbalimbali zikiwemo utalii, kilimo, elimu, michezo, ufugaji, uvuvi , biashara na ujasiriamali.
Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipofungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC) Mei 17 2024.
Amesema matarajio yake ni kuona taasisi nyingi za umma kutoka Zanzibar zinawekeza katika benki ya CRDB ili kuendelea kuipa nguvu zaidi kuwezesha ushiriki wake katika miradi ya maendeleo.
Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa mmoja wa wanahisa wa CRDB kupitia Mfumo wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), inajivunia sana utendaji wa CRDB.
Amewakwa pongeza Benki ya CRDB kwa mafanikio waliyopata katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa mkakati mpya wa biashara.
Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa wanahisa kutumia vyema fursa ya kujifunza kupitia semina hii .
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema CRDB itakuwa mdau muhimu wa maendeleo ya Zanzibar na kuendelea kutoa ushirikiano.