Home AFYA NEMC IMETOA SIKU 90 KWA KUWEKA MIUNDOMBINU SAHIHI KWA TAASISI...

NEMC IMETOA SIKU 90 KWA KUWEKA MIUNDOMBINU SAHIHI KWA TAASISI ZOTE NCHINI ZINAZOJISHUGHULISHA NA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku 90 kwa kuweka miundombinu sahihi kwa taasisi zote nchini zinazojishighulisha na utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya mazingira na kanuni zake kwa kuacha utupaji taka hovyo.

Akizungumza leo Mei 16 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa NEMC, Hamad Kissiwa amesema ukiukwaji wa matakwa ya sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake juu ya usimamizi na utupwaji wa taka hatarishi zitokanazo na huduma ya afya.

Ameeleza kuwa taka hatarishi zinatokana na huduma ya afya ni pamoja na madawa yaliyotumika , taka zenye mgando wa damu, sehemu za mwili wa binadamu zilizoondolewa sababu za magonjwa mbalimbali taka zenye viambukizi vya magonjwa,vitu vyenye nchi kali na zinginezo

“Taasisi za huduma ya afya kufuata sheria ya mazingira na kanuni zake pamoja na miongozo ya wizara ya afya tahadhari tunatoa kwa yeyote anaeyejishughulisha na shughuli hizi kuacha mara moja utupaji taka ovyo zitokanazo na huduma ya afya hivyo ndani ya siku 90 kuweza kujisajili kwenye wizara husika ili kupata utaratibu mzuri kupata vibali maalum vya usimamizi wa taka hizi,”amesema Kissiwa.

Amesema taka hizo ni hatarishi kwa afya ya binadamu, viumbe hai na mazingira kama hazitaratibiwa na kusimamiwa ipasavyo ili kuzuia na kudhibiti athari hizo zitokanazo na taka zenye madhara zitokanazo na huduma ya afya.

“Kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na taarifa na kushuhudiwa n ukusanyaji, usafirishaji na utupaji taka holela wa taka zitokanazo na huduma ya afya katika maeneo mbalimbali nchini.

“Hivyo ni dhahiri kuwa kuna baadhi ya watoa huduma za afya wasio waaminifu ambao wanakiuka matakwa ya sheria ya usimamizi wa mazingira sura ya 191 na kanuni zake kwa kusafirisha na kutupa taka ovyo zitokanazo na huduma ya afya bila kufuata utaratibu uliowekwa na sheria na wizara ya afya,”ameongeza

Amesema mfumo mahsusi unaofanya kazi kwa ufanisi kwa kudhibiti taka hizo unapaswa ufuatwe kama ilivyobainishwa kwenye sheria ya usimamizi wa mazingira Sura ya 191 na kanuni za udhibiti wa taka hatarishi ya mwaka 2021.

Aidha amesema Baraza limezielekeza mamlaka za udhibiti nchini zinazoshughulikia usimamizi wa taka zitokanazo na huduma ya afya kuhakikisha kwamba waatoa huduma hizo nchini kote wanafuata miongozo iliyowekwa na wizara pamoja na masharti na kanuni za udhibiti na usimamizi wa taka zao uliowekwa na sheria na wizara ya afya.

Kissiwa amesema wanatarajia kufanya ukaguzi kupitia kanda zao zote ili kubaini wanaoenda kinyume na sheria kuanzia vituo vya afya, zahanati na hospitali kuu huku wanaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here