Na Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake Tanzania(UWT), Mary Chatanda amewahimiza Wakandarasi wanawake kuchangamkia Fursa ya Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili waweze kuimarisha mitaji na ufanisi wa kazi zao, hatua ambayo itawawezesha kuaminiwa zaidi na hata kukabidhiwa miradi mikubwa zaidi ya kitaifa.
Chatanda ameyasema hayo Leo Mei 16, 2024 wakati wa kikao cha wakandarasi Wanawake kilichofanyika Makao makuu ya UWT Dodoma.
“Tulipozungumza kwa mara ya kwanza katika Kikao chetu mlisema Kuna changamoto ya mitaji katika makampuni yenu sasa Rais Samia amesikia kilio chenu na ndio maana nawahamasisha wakandarasi wote wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo hii.
“UWT imefurahi kuona wakandarasi wanawake wanapata tenda kwenye miradi mbalimbali katika Wilaya na Mikoa nchi nzima,hii ni moja ya juhudi za UWT kuhakikisha wanawake wanapata tenda za Ujenzi wa Barabara kwa wingi,”amesema.