Home KITAIFA MTUTWA AMEWATAKA WANANCHI KILIPA KODI YA ARDHI KWA WAKATI

MTUTWA AMEWATAKA WANANCHI KILIPA KODI YA ARDHI KWA WAKATI

Na Mwandishi wetu, Mwanza

KAMISHINA Msaidizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi Mkoa wa Mwanza, Happiness Mtutwa amewataka wananchi wa mkoa huo kulipa Kodi ya Ardhi Kwa wakati

Akizungumza Mei, 13 2024 na waandisi wa habari Mtutwa amesema wananchi wengi wanachanganya kodi ya ardhi na kodi ya majengo, hivyo wananchi wanatakiwa kujua kodi ya ardhi Inalipwa ofisi za ardhi za mkoa, Halmashauri na Wilayani , kodi za majengo zinalipwa TRA kupitia njia ya Luku.

“Ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi ya kampuni, viwanja, taasisi za umma na binafsi kutolipa Kodi za ardhi kunaweza kupelekea kunyanganywa eneo lako,lakini pia kufikishwa mahakamani ambapo unaweza kufutiwa umiliki wa hati yako,”amesema Mtutwa

Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza walipe kodi ya ardhi Kwa wakati Ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Aidha amewajulisha kuwa Migogoro ya ardhi mkoa wa Mwanza imepungua Kwa kiasi kikubwa sana yote ni mafanikio ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewaombe wananchi wa mkoa wa Mwanza walipe kodi kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here