Home KITAIFA SERIKALI KUUNDA KAMATI MAALUM KUSHUGHULIKIA HOJA ZA CAG KILA MWAKA -DK.MWINYI

SERIKALI KUUNDA KAMATI MAALUM KUSHUGHULIKIA HOJA ZA CAG KILA MWAKA -DK.MWINYI

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itafanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG na kuunda kamati maalum itakayoshughulikia kasoro za kiutendaji zinazotokana na hoja za CAG kila mwaka.

Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said kuunda kamati hiyo.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo baada Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Dk.Othman Abbas Ali kuwasilisha ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2022/23 iliyofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar Mei, 132024.

Amesisitiza kuendelea kuheshimiwa Ofisi ya CAG na kutoingilia kwa mujibu wa katiba katika kutimiza majukumu yake kwa uhuru.

“Nimeridhika kwa hatua za mafanikio ya zaidi ya asilimia 90 ya hati za ukaguzi zinazoridhisha katika ripoti ya mwaka 2022/23,” amesema Dk.Mwinyi

Amebainisha kuwa Serikali ikijikita kujiendesha kwa njia ya mifumo ya kidijitali katika kila nyanja itasaidia kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here