Home KITAIFA TUENDELEE KUIOMBEA NCHI NA VIONGOZI WAKE-DK.MWINYI

TUENDELEE KUIOMBEA NCHI NA VIONGOZI WAKE-DK.MWINYI

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwaombea Dua Viongozi ili watimize majukumu yao na kutekeleza ahadi walizoahidi.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Qubaa Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Mei 10 2024.

Pia Rais Dk.Mwinyi amewatembelea Wazee akiwemo Mbunge wa zamani Jimbo la Amani , Mzee Hassan Rajab nyumbani kwake Kisauni na Mjumbe wa Baraza la Wazee CCM Kisiwandui, Bi Maryam Hengwa nyumbani kwake kwa Mchina Mkoa wa Mjini Magharibi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here