Home KITAIFA WADAU WA KILIMO WAIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU NA MITAJI KWA VIJANA.

WADAU WA KILIMO WAIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU NA MITAJI KWA VIJANA.

Na Sophia Kingimali@Lajiji Digital

KATIKA kuendelea kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuleta tija kwa wananchi Jukwaa la wadau wa kilimo wasio kuwa wa kiserikali(ANSAF)wametoa rai kwa serikali kuhakikisha katika bajeti iliyopitishwa ya wizara ya kilimo 2024/2025 wanatenga pesa kwa ajili ya kutoa elimu kwa vijana lakini pia kuwapa mitaji kwa ajili ya kuingia kwenye kilimo.

Akizungumza wakati akitoa wasilisho la bajeti ya wizara ya kilimo katika jukwaa la wadau kijinsia DGSS-TGNP Mei 8,2024 jijini Dar es Mwakilishi wa ANSAF Werner Hillary amesema ni muhumu kama wananchi kujua bajeti ya wizara hiyo kwani ni muhimu katika uchumi wa nchi.

“Nimekuja hapa ili kuhakikisha wote tunapata uwelewa wa kujua kimepangwa nini kinatekelezwa kipi na vipaumbele ni vipi ili kila mtu aweze kuielewa na kutoa maoni wapi kwenye mapungufu na wapi pa kuboresha”,amesema.

Amesema pamoja na serikali kuja na mfumo mzuri wa kuhakikisha vijana wanaingia katika kilimo ambapo wamekuja na BBT ila wanapaswa kuangalia namna ya kuwasaidia vijana ambao hawapo kwenye mfumo wa BBT hasa wale waliopembezoni na wanaojihusisha na kilimo.

Wena amewataka vijana kuchangamkia fursa pindi zinapojitokeza na kujitahidi kutafuta taarifa ili waweze kushiriki katika fursa hizo.

“Mimi naamini asilimia kubwa ya vijana wanatumia simu janja hivyo ni vyema kuzitumia vizuri katika kutafuta fursa ambazo zipo na watu awazichangamkii,”mesema.

Kwa upande wake Mzee Hamis Masanja Katumwa amesema pamoja na elimu kutolewa serikali inapaswa kuzingatia jinsia pindi wanapowachagua vijana na wanawake katika BBT kwani mfumo uliopo uliopo wanaume wengi ndio wamepata nafasi kuliko wanawake.

“Tunaiomba serikali hao wanaowapeleka kwenye huo mradi wa BBT uzingatie jisia wanawake wengi wamekuwa wakiachwa kutokana na majukumu ya malezi lakini wakitengeneza mazingira mazuri ya mtu kufanya kilimo mahari alipo na awazeshwe sawa na wengine,”amesema Katumwa.

Nao washiriki katika jukwaa hilo DGSS wametao rai kwa serikali ili kuhakikisha vijana wengi na wanawake wanaingia kwenye kilimo kwa kuwahakikishia wanatoa elimu kwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ya kutumia tehama ambapo ndio vijana wengi wanatumia katika kupata taarifa na elimu mbalimbali.

Wamesema serikali inaposema bajeti imeongezeka inapaswa ioneshe kwa vitendo kwa kupunguza gharama za bidhaa kwa wananchi lakini pia kurahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wananchi ili kuendelea kuhamasisha kilimo.

“Mnapotuambia bajeti imeongezeka sisi kama wananchi tunaipima kwenye mahitaji yetu mwaka huu tulishanunua mchele mpaka 4000 na sukari mpaka 5000 tunaiomba serikali bajeti iwekwe inayotekelezeka na sio bajeti kubwa isiyotekelezeka,”mesema Hancy Obote mmoja wa washiriki.

Wakizungumzia mbolea za Ruzuku wameiomba wizara kuangalia namna ya kupunguza ufungashaji wa mbolea kwa kuzingatia mahitaji ya watu kwani sio wote wanaomudu kununua kilo 25 wengine wanamashamba madogo.

Pia,wameiomba kuangalia upya lugha inayotumika katika mifuko ya mbolea hiyo kuweza kubadilishwa na kuandikwa kwa kiswahili ili kumuwezesha kila mkulima kuweza kuelewa maelekezo yaliyowekwa kwenye mifuko hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here