Home KITAIFA DK. KIJAJI ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA...

DK. KIJAJI ANATARAJIA KUWA MGENI RASMI SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MILIKI UBUNIFU DUNIANI.

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji anatarajia kuwa mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu Duniani yanayotarajiwa kufanyika Mei 9,2024 jijini Dar es salaam ambapo maazimisho hayo yataenda na utaiji saini wa hati ya makubaliano katika eneo la miliki ubunifu baina ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) na COSOTA.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 8,2024 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Miliki Bunifu wa BRELA, Loy Mhando Amesema maadhimisho hayo yalianzishwa na Shirika la miliki ubunifu Duniani (WIPO) Ambapo yatafanyika katika Hotel ya Johari rotana huku kauli mbiu ikiwa “Miliki Ubunifu na malengo ya Maendeleo endelevu Kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia Ubunifu”.

“Maadhimisho ya siku ya Miliki Bunifu Duniani huadhimishwa Aprili 26 kila mwaka lakini kwa hapa kwetu kutokana na Tarehe hiyo kuwa na jambo muhimu la kitaifa la kuazimisha muungano sisi tunaazimisha siku tofauti ambapo mwaka huu tunaadhimishia tarehe Mei, 9 2024,”amesema.

Ameongeza kuwa katika maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana nayo ikiwemo mijadala kuhusu Miliki Ubunifu ambayo itahusu fursa,mafanikio na changamoto wanazokutana nazo katika nyanja nzima ya miliki ubunifu.

“Vile vile, hati za makubaliano ya ushirikiano katika eneo la Miliki Ubunifu baina ya BRELA,COSOTA na Taasisi nyingine zitasainiwa ikiwa ni njia ya kurasimisha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi hizo katika kuhakikisha Miliki Ubunifu inaleta manufaa katika maendeleo ya kiuchumi na teknolojia nchini,”amesema.

Amesema Miliki Ubunifu inatija kubwa kwa wabunifu kwani inawapa ulinzi wa kumiliki bunifu zao na kuwasaidia katika kupata haki zao endapo mtu yoyote ataingilia ama kutumia bunifu yake pasipo makubaliano na mmiliki.

Mashirika ya kimataifa na kikanda ya Miliki Ubunifu yameongeza wigo wa ulinzi wa bunifu za wabunifu katika maeneo mbalimbali Duniani hususani kwa wabunifu wa kazi zinazovuka mipaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here