Home KITAIFA CCM IMEAMUA KUTOA ELIMU KUHUSU MASUALA YALIYOPO MAHAKAMANI – MAKALLA

CCM IMEAMUA KUTOA ELIMU KUHUSU MASUALA YALIYOPO MAHAKAMANI – MAKALLA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Amos Makalla amesema kuwa viongozi wengi wa chama wamekuwa wakipokea ujumbe kutoka kwa watu mbalimbali kupitia simu na hata malalamiko kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara kuhusiana na kesi ambazo tayari zilishatolewa maamuzi na mahakama.

Kutokana na hayo, Makalla ameeleza kuwa CCM inaamini katika utawala bora wa kuzingatia vyombo vya sheria na kuwa haki ya kutoa haki inapatikana kupitia Mahakama na hakuna mwenye mamlaka ya kuingilia mahakama.
Makalla ameyasema hayo leo akiwa kwenye kipindi cha #Goodmorning# kinachoruka kupitia redio ya wasafi, alipotembelea katika studio za Wasafi Media ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapa Nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here