Na Mwandishi wetu, Iringa
IKIWA ni muendelezo wa utekelezaji wa dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha sekta ya afya na kusogeza huduma bora kwa Wananchi, Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amezindua rasmi mpango kabambe wa Madaktari Bingwa wa Rais Samia mkoani Iringa katika Hospitali ya Frelimo Manispaa ya Iringa.
Akizungumza Mei ,6, 2024 mkoani humo wakati uzinduzi huo Ummy ameeleza kuwa mpango huo muhimu na maalumu utasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa kuwajengea uwezo wahudumu katika hospitali za wilaya, kwakuwa dhamira ya serikali nikuwa na wodi maalumu za watoto wachanga katika hospitali hizo ili kuokoa maisha ya watoto wachanga wenye siku 0-28.
Ummy ameeleza kuwa ujio wa madaktari hao bingwa utasaidia kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi, utasaidia kubadilishana uzoefu na wahudumu katika ngazi za wilaya, Itapunguza gharama na umbali kwa wananchi wa hali ya kawaida kuifuata na kuigharamia huduma hiyo.
Akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mkuu wa wilaya ya Iringa, Kheri James amawaelekeza viongozi wa ngazi zote kuwataarifu Wananchi juu ya fursa hiyo muhimu ili wajitokeze, na amewataka viongozi na watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kuwapa ushirikiano madaktari hao Bingwa kwa siku zote tano watakazo kuwepo katika mkoa wa Iringa.
Zoezi la huduma za kibingwa katika mkoa wa Iringa litafanyika kwa siku tano katika Hospitali zote za Halmashauri za mkoa wa Iringa.
#Iringa Imara,Tutaijenga kwa umoja na uwajibikaji.