Home KITAIFA RAIS SAMIA AAGIZA HUDUMA ZA DHARURA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA KIMBUNGA HIDAYA

RAIS SAMIA AAGIZA HUDUMA ZA DHARURA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA KIMBUNGA HIDAYA

Na Mwandishi wetu, Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ameagiza huduma za dharura zipelekwe kwenye maeneo yaliyopata athari kutokana na kimbunga Hidaya.

Hayo yamesemwa leo Mei 6, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Maafa Kitaifa alichokiitisha kupokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa kwenye maeneo yaliyopata athari.

“Rais ameelekeza hatua za haraka zichukuliwe katika maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua zilizotokana na athari za kimbunga Hidaya ikiwa ni pamoja na kupeleka misaada,” amesema. Maeneo yatakayopelekewa misaada hiyo ni Mafia mkoani Pwani, Kilwa (Lindi) na Ifakara (Morogoro).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here