Na Mwandishi wetu, Biharamulo
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 03 Mei, 2024 amezindua Kituo cha Afya na kushuhudia pia makabidhiano kati ya Wizara na Kikosi cha Majengo ya kuishi Maafisa na Askari.
Amesema Kituo hicho cha Afya ni muhimu na hatua ya kujivunia kwani kitatoa huduma za tiba kwa wanajeshi, familia za wanajeshi na wananchi wanaoishi maeneo jirani.
Akizungumza Mei, 3,2024 Maafisa na Askari pamoja na raia mara baada ya uzinduzi huo, Waziri Tax amemshukuru kwa dhati Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
“Namewapongeza viongozi, maafisa na maaskari waliosimamia na kushiriki katika ujenzi huu kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa vigezo na kuzingatia thamani ya fedha.Dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWT) kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma zinazohitajika,” amesema Dk. Tax.
Pia amewashukuru pia Maafisa na Askari kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwa kujituma, weledi na uhodari katika utekelezaji wa majukumu yao na akasisitiza umuhimu wa kusimamia na kutunza majengo yaliyozinduliwa, vifaa tiba na visima vilivyokabidhiwa ili vidumu na kuendelea kutoa huduma bora kwa muda mrefu.
Aidha, Dk. amemshukuru Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama na taasisi zote za Serikali zilizoshiriki na kufanikisha ujenzi wa miradi hiyo, na kuwataka kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha ulinzi na huduma kwa ustawi wa wapiganaji na raia kwa ujumla.
Kabla ya kuzindua rasmi jengo la la Kituo cha Afya cha K-9 Dk.Tax alipata fursa ya kutembelea jengo hilo na kupata maelezo na kupanda mti wa kumbukumbu katika eneo la zahanati.