Na Mwandishi wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Mary Chatanda (MCC) amezielekeza Halmashauri zote Nchini, kuhakikisha Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri iwafikie walengwa hususani wafanyabiashara Wanawake wadogo wadogo ili waweze kujiinua kiuchumi.
Mwenyekiti Chatanda ametoa agizo hilo leo Mei 04, 2024 Baada ya Mwenyekiti wa Wanawake wauza mboga na Matunda jijini Dodoma Mama Chacha kuwasilisha changamoto ya wafanyabiashara kukosa mikopo,na kuwa na dhana kuwa mikopo hiyo ni kwa watu maalum tu. na sio wanawake wote pamoja na uwepo wa mikopo kandamizi kwa wanawake ijulikanayo “Kausha Damu” ambayo imekuwa mwiba kwa wanawake wauza mboga mboga kujiendeleza kiuchumi.
“Kulikuwa na Changamoto ya mikopo ya Halmashauri kutowafikia walengwa Husika, Naelekeza Halmashauri Zote Nchini zitoe Mikopo kwa Wanawake wote walengwa wanapata mikopo hiyo bila kupindisha pindisha.
Natoa Rai kwa Serikali kuidhibiti au Kusitisha kabisa Mikopo ya Kausha Damu, Ujinga haushi nk kwani inawaumiza wanawake wengi sana,” amesema Chatanda.
Chatanda amesema hayo wakati wa Kongamano lililojumuisha wafanyabiashara wanawake wa mboga na Matunda takribani 3000 lililoandaliwa na SHIM Media Company Limited kwa Ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .