Home KITAIFA ZINGATIENI TAARIFA ZA TMA – WAZIRI JENISTA MHAGAMA

ZINGATIENI TAARIFA ZA TMA – WAZIRI JENISTA MHAGAMA

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WANANCHI wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa na kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri na tahadhari kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) pamoja na kupata ushauri wa kina na miongoz ya kitaalam kutoka Sekta husika ili kuweza kujikinga na adhari zinazoweza kujitokeza.

Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 3, 2024 Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama.

Waziri Jenista amezielekeza mamlaka za Mikoa husika kuumendelea kuchukua tahadhari za kutosha na kuendelea kutoa taarifa zinazohusiana na mwenendo wa ‘KIMBUNGA HIDAYA’ ili kuchukua hatua stahiki pale dalili zinazoashiria na kuelezea na mamlaka ya hali ya hewa zitakapoendelea kujitokeza.

“Nitoe rai kwa Taasisi zinazohusika katika ngazi za Mikoa, Wilaya, Kata na mpaka maeneo ya mitaa na vijiji kuendelea kuchukua tahadhari na kufuatilia kwa karibu sana taarifa hizi za mamlaka ya hali ya hewa Nchini,”amesema Mhagama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here