Home KITAIFA WIZARA YA KILIMO YAHITIMISHA BAJETI YAKE KWA KISHINDO MEI 03, 2023

WIZARA YA KILIMO YAHITIMISHA BAJETI YAKE KWA KISHINDO MEI 03, 2023

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WIZARA ya Kilimo imehitimisha bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Bungeni jijini Dodoma kwa kishindo kikubwa.

Bajeti hiyo ya zaidi ya shilingi Trilioni 1.24 inatajwa kubeba matumaini ya mamilioni ya wakulima na watanzania wote kwa ujumla.

Akiwasilisha bajeti hiyo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuleta mageuzi katika Sekta ya kilimo kwa kukifanya kilimo kuwa na tija zaidi katika uzalishaji wa mazao na kupanua wigo wa ajira zenye staha pamoja na utafutaji wa masoko.

Wizara ya kilimo imelenga kutengeneza mazingira ya wakulima kuzalisha zaidi chakula cha kutosha nchini na kulisha wengine kibiashara, hivyo Wakulima wamehimizwa kubadilika na kuishi katika falsafa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here