Home KITAIFA KIKAO CHA PAMOJA CHA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA MAMBO...

KIKAO CHA PAMOJA CHA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA MAMBO YA ULINZI, USALAMA NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) Aprili 30, 2024 jijini Dar-es-Salaam aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha pamoja cha 12 cha Baraza la Kisekta cha Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaohusika na masuala ya Ulinzi, Usalama na Mahusiano ya Kimataifa. Pamoja na masuala mengine kikao kiliidhinisha Mkakati wa Pamoja wa Ushirikiano baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Faraji Kasidi Mnyepe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Balozi Stephen Mbundi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maafisa toka Sekta husika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here