Na Mwandishi wetu, Morogoro
WAKAZI 6,453 wa vijiji vya Mngazi na Dakawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wanatarajia kunufaika na mradi wa uhifadhi wa chanzo cha mto Mngazi,Mgeta na Ruvu kupitia ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji uliopo halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.4 wamesema unaenda kutatua changamoto ya kuchangia matumizi ya maji baina ya binadamu na wanyama hali ambayo ilikuwa inachangia kuwepo kwa magojwa ya milipuko hii ni baada ya kuwekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Eliakim Mnzava
Lengo la Mradi huo ni kutunza hifadhi ya Mto Ruvu ambao unatagemewa na Mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Pwani, aidha mradi huo utapunguza uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na shughuli za kibinaadamu zinazofanyika pembezoni mwa chanzo hicho.