Home KITAIFA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NAIROBI-KENYA

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NAIROBI-KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Wimbo wa Taifa wa Kenya pamoja na ule wa Umoja wa Afrika (AU) ukiimbwa kabla ya kuanza Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba alihudhuria mkutano huo. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya Aprili, 29 2024

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Natu El Maamry Mwamba, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), uliofanyika Aprili, 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri wa Fedha,Dk. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Natu El Maamry Mwamba, na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mary Kamari (kushoto), baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), uliofanyika Aprili, 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya. 

Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Zanzibar Dk. Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Natu El Maamry Mwamba, (katikati) Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru (wa kwanza kulia), Kamishna wa Fedha za Nje, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Zanzibar, Yussuf Ibrahim Yussuf baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), uliofanyika Aprili, 29 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here