Na Mwandishi wetu, Saudi Arabia
SERIKALI imewakaribisha wafanyabiashara wa Saudi Arabia kuja kufanya Biashara Tanzania katika sekta za Kilimo, Viwanda, Mifugo, Nishati, Madini, Utalii, Madawa na Miliki ya Ujenzi (Real Estate).
Wafanyabiashara hao wamekaribishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji akiwa na ujumbe wake Aprili 29, 2024 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Saudi Arabia, Hassan Al-Huwaizi, wakati waMkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Naye Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara na Viwanda ya Saudi Arabia, Hassan Al-Huwaizi na ujumbe wake ameridhia kuwaunganisha wanyabiashara na wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuja kuwekeza Tanzania.
Aidha, kwa upande wa Tanzania, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake za WRRB na TANTRADE wameonesha uhakika wa kutoa ushirikiano mkubwa kwa kushirikiana na taasisi za sekta husika pamoja na Kituo cha Uwekezaji.
Dk. Kijaji aliongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliowajumuisha Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha ,Rashed Bade, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Sempeho Manongi, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maghala,Asangye Bangu, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Deo Shayo, na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, Saudi Arabia