Home AFYA MSD WAMEKUBALIANA KUSHIRIKIANA NA BOHARI YA DAWA YA SIERRA LEONE

MSD WAMEKUBALIANA KUSHIRIKIANA NA BOHARI YA DAWA YA SIERRA LEONE

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

BOHARI Kuu ya Dawa Nchini (MSD) wamekubaliana kushirikiana na Bohari ya Dawa ya Sierra leone kubadilishana taarifa za utendaji ili kuwasaidia bohari hiyo kuweza kukua na kufikia ukubwa wa MSD.

Akizungumza leo Aprili 29,2024 wakati wa mazungumzo na ugeni kutoka Sierra Leon uliokuja nchini kujifunza shughuli zinazofanywa na MSD Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kutokana na utendajikazi wa bohari hiyo umeendelea kuvutia wengi kuja kujifunza.

Amesema moja ya kitu kilichowavutia zaidi ni ubunifu ambao MSD wamekuwa nao katika kufanya shughuli zao za kununua na kusambaza dawa lakini pia uhimilivu wa fedha lakini na matumizi ya Tehama.

“Tunakumbuka Sierra Leon ni nchi ambayo ilikubwa na matatizo ya amani ambao ulivunja vunja mfumo mzima wa afya sasa wameamka na kujikung’uta na kuanza upya mfumo wao wa afya na sasa wamekuja huku kujifunza namna ya sisi tunavyofanya kazi zetu.

Amesema watawasaidia taasisi yao jinsi ya kuweza kushirikiana na wadau wengine ndani ya serikali na nje ya serikali ikiwemo kuunganisha mifumo yao na idara mbalimbali, kama watu wa fedha, utumishi, wateja na wizara ya afya.

Kwa upande wake,Mfamasia Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Huduma za Dawa Nchini, Daud Msasi amesema ujio wa wageni hao ni kuona wanaboresha bohari yao ya dawa inaboreshwa na kuimarika katika kutoa huduma.

“Ukiona mtu amechambua akaja akaswma akajifunze Tanzania inamaanisha tunafanya vizuri na ndio maana ndugu zetu hawa wakachagua kuja hapa kujifunza ni ugeni mzito ambao umeongozwa na Mganga mkuu wa nchi yao,” amesema.

Amesema nchi ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi wa Afrika.

Naye Mfamasia Mkuu na Mkurugenzi wa huduma za Kifamansia Wizara ya Afya Sierra Leon, Dk.Moses Batema amesema wamefanya utafiti wa kutosha na kuona sehemu ya kwenda kujifunza ni Tanzania hivyo wameridhishwa na majadiliano walioyafanya lakini pia wamejifunza vitu vingi vitakavyowasaidia kuboresha Bohari yao.

Naye Naibu  Mkurugenzi wa  Uendeshaji  Wakala wa Taifa wa Usambazaji wa Dawa wa Sierra Leone,  Jatu Abdulai amesema  matumaini yake ni kuwa kati ya bohari za dawa hizo mbili wamebadilishana ujuzi katika masuala ya usambazaji wa dawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here