Home KIMATAIFA DK. KIJAJI ATETA NA SAUDA EXIM

DK. KIJAJI ATETA NA SAUDA EXIM

Na Mwandishi wetu, Saudi Arabia

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji ameishauri Benki ya Saudi Exim kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia ili waweze kuongeza mitaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali nchini na kukuza biashara baina ya nchi hizo.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Saudi Exim, Mhandisi Saad Alkhalb.
Aprili 28, 2024 sambamba na Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.

Aidha Dk. Kijaji ameialika SAUDI EXIM kutembelea Tanzania ili kuwezesha Biashara baina ya nchi hizi mbili kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wakandarasi wanaotekeleza kazi zao nchini Tanzania na wafanyabiashara

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Saudi Exim, Mhandisi Saad Alkhalb ameahidi kufanyia Kazi fursa zilizopo kati ya Tanzania na Saudi Arabia ili kuwezesha mitaji na ufanisi wa ufanyaji biashara kwa manufaa zaidi hususani katika nyama samaki na matunda.

Dk. Kijaji anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaowajuisha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Sempeho Manongi, Mkurugenzi wa Bodi ya Maghala, Asangye Bangu, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Deo Shayo, Kamishna wa Fedha za Nje, Rashed Bade na Maafisa Waandamizi wa Ubalozi wa Tanzania- Riyadh Saudi Arabia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here