Home MICHEZO RAIS DK.MWINYI AWAKABIDHI SIMBA UBINGWA WA MUUNGANO

RAIS DK.MWINYI AWAKABIDHI SIMBA UBINGWA WA MUUNGANO

Na Mwandishi wetu,Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amewakabidhi timu ya Simba shilingi milioni 50 ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Muungano kwa mwaka huu katika uwanja wa New Amaan Complex tarehe 27 Aprili 2024.

Timu ya Simba imeifunga goli moja kwa sifuri timu ya Azam.

Aidha Mashindano hayo yamerejea tena nchini ikiwa ni shamrashamra za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Miaka 20 imepita tangu kusimama kwa mashindano hayo ambayo yamemalizika kwa kushirikisha timu za Zanzibar na Tanzania Bara ikiwemo Simba, Azam, KMKM na KVZ.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here