Home KITAIFA DK. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA IDA21 JIJINI NAIROBI-KENYA

DK. NCHEMBA ASHIRIKI MKUTANO WA IDA21 JIJINI NAIROBI-KENYA

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba akipokelewa na Waziri wa Fedha wa Kenya Profesa Njuguna Ndung’u, alipowasili kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika Aprili, 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum, akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Natu El Maamry Mwamba, (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wa Kenya, Dk. Chriss Kiptoo, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika Aprili, 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya. 

Waziri wa Fedha, Dk.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godogwana, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika Aprili, 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.

Waziri wa Fedha,Dk. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Waziri wa Mipango wa Angola, MVictor Hugo Guiherme, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika Aprili, 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum, na Kamishna wa Fedha za Nje Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Yussuf Ibrahim Yussuf (katikati) na  Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Noel Kaganda, wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika Aprili 28 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here