Home KITAIFA TET YAKABIDHI VITABU VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 7 WILAYA...

TET YAKABIDHI VITABU VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 7 WILAYA YA KIBITI

Na Mwandishi wetu, Kibiti

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imekabidhi vitabu vya kusomea 422 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7 kwaajili ya Shule tatu zilizofungwa kwa kuathiriwa na maji ya mafuriko ya Mto Rufiji huko Wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumza Aprili 25, wakati wa kukabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Hemed Magaro kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph kolombo kwa upande wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Mkuu wa kitengo Cha Elimu maalumu wa wizara hiyo Dk. Magreth Matonya amesema vitabu hivyo wameleta kwa Shule walizobaini kwamba watoto hawaendi shule wamefunga na vifaa vyao vyote vilichukuliwa na maji ya mafuriko.

Alisema awali walileta vifaa vyote vya kujikimu mtoto katika kujisomea lakini TET wameleta vitabu vya kusomea ambavyo vitasaidia mwalimu na mwanafunzi waweze kufundishana kwenye mahema au kwenye shule maalumu zilizochaguliwa kwaajili ya kuwastili watoto walipata changamoto za mafuriko.

Dkt. Matonya amesema Kuna vitabu 121 vya Delta shule ya msingi, vitabu 181 vya Usimbe shule ya msingi, vitabu 122 vya Shule ya msingi Nyambele.

“Tumeleta vifaa vya Shule ikiwa ni pamoja na mahema kwaajili ya wao kukaa darasani, vifaa vya kuandikia na madaftari na Sasa tunamaliziia kuleta vitabu kutoka TET,”amesema Dk. Matonya.

Naye Mfanyakazi wa TET, John Ngowi amesema walipokea maelekezo ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Aldof Mkenda na wameleta vitabu hivyo kwaajili ya wanafunzi walioshindwa kuhudhuria vipindi vya masomo yao kwasababu ya mafuriko ya Mto Rufiji yaliyowakuta na kuzoa vitatu vyao.

Amesema vitabu vilivyoletwa ni vya kufundishia kwa madarasa yote ya msingi kwa shule hizo tatu vyenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 7 na taasisi hiyo bado ipo tayari kuendelea kushirikiana na Wilaya hiyo kutatua changamoto hiyo.

John amesisitiza matumizi bora na sahihi ya vitabu hivyo wasivihifadhi kwenye kabati bali watumie kwaajili ya kupata maarifa zaidi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Hemed Magaro ameishukuru TET kwa msaada huo ambapo shule zilizotajwa walilazimika kuzifunga kwasababu ya kuwaepusha na athari za mafuriko hayo.

“Kwa Kweli tumelazimika kuzifunga kwasababu haiwezekani tena watoto kusoma pale na watoto hao tuna mpango wa kuwachukua na kuwapeleka kwenye shule ya msingi Kitundu ambako tuna baadhi ya mabweni ambayo tutaweka watoto na kuna mahema tumepata hivyo watoto wanaweza kuishi pale ili kupata elimu na tuna chakula tutatumia kwaajili ya watoto hao,” amesema Magaro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here