Home KITAIFA WANAWAKE WANA MCHANGO MKUBWA KATIKA MUUNGANO WETU DK.MWINYI

WANAWAKE WANA MCHANGO MKUBWA KATIKA MUUNGANO WETU DK.MWINYI

Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Wanawake walikuwa na mchango mkubwa kufanikisha kufanyika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuzingatia tulipotoka, tulipo na tunakolekea katika harakati za historia ya nchi yetu .

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika Mdahalo wa kutathimini Nafasi ya Mwanamke wa Tanzania katika Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam t Aprili,25 2024.

Ameipongeza UWT kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutekeleza mambo mbalimbali yenye lengo la kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na kukiunganisha Chama na wananchi.

“Muungano wa Tanzania umeleta faida nyingi za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano,”amesema Dk.Mwinyi.

Ameeleza kuwa dhamira njema ya Waasisi wa Taifa letu ya kuunganisha nchi zetu mbili imeendelezwa na Viongozi wa pande zote mbili za Muungano kwa kuudumisha, kuimarisha kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza hadi sasa na hivyo kuufanya uwe imara zaidi.

Dk.Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kujiandaa vya kutosha ushiriki wao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa upande wa Tanzania Bara mwaka huu na Uchaguzi mkuu mwakani 2025 katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano

Vilevile amehamasisha wanawake kushiriki kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali wakati wa chaguzi zitakapofikia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here