Home KITAIFA UNICEF WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI NA WALIMU KWA...

UNICEF WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI NA WALIMU KWA SHULE ZILIZOATHIRIKA NA MAFURIKO KIBITI NA RUFIJI

Na Scolastica Msewa, Rufiji

SHIRIKA la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) limetoa msaada wa vifaa vya Shule za msingi na sekondari zilizoathirika na mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani ambapo wanafunzi 1040 na Walimu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 9586.20 .

Wakati akikabidhi Msaada huo Aprili 24 Mkuu wa kitengo Cha Elimu maalumu wa wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Magreth Matonya kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ambaye aliwakirishwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amesema vifaa vilivyotolewa ni kwaajili ya shule 14 zilizoathirika na mafuriko kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti.

Amesema Msaada huo utapelekwa kwenye shule hizo ambazo maji ya Mto Rufiji yamejaa ambapo Wanafunzi hawawezi kuendelea na masomo na vifaa vyao vimeharibika kwa namna Moja au nyingine na mafuriko hayo yanayoendelea wilayani humo.

Dkt. Matonya ametaja aina ya vifaa hivyo vya Shule vilivyoletwa kuwa ni pamoja na mahema ya kutengeneza madarasa 4, vifaa vya kusomea wanafunzi, vifaa vya kufundishia kwa walimu, vifaa vya michezo na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Amesema katika mahema hayo matatu yatapelekwa kwaajili Shule 7 zilizofungwa wilaya ya Rufiji na hema moja litakabidhiwa kwaajili ya Shule zilizofungwa wilayani Kibiti.

Akipokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele ameishukuru UNICEF kwa msaada huo na Wilaya ya Rufiji na Kibiti Ina shule 23 zilizoathirika na mafuriko hayo huku shule 14 zimefungwa kwa athari za mafuriko hayo kwa Wilaya zote mbili.

Akipokea Msaada huo kwaajili ya Wilaya ya Kibiti Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph kolombo ameishukuru serikali na wizara ya Elimu, UNICEF kwa msaada huo na kwamba vifaa hivyo vitasaidia Wanafunzi wa shule wa S tatu wilizofungwa kabisa kwasababu ya mafuriko hayo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Simon Belege amesema misaada hiyo itasaidia wanafunzi wenye mitihani ya kitaifa kuendelea na masomo ili wasipitwe na kuchelewa muda wa mitihani ya kittaifa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti,Hemed Magaro aamesema haraka wanajenga mahema hayo ili wanafunzi waendelee na masomo yao kwa kutumia vifaa hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rufiji Kaswakala Mbonde ameonya wanaosema mafuriko hayo ni kutokana na kujengwa kwa Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwani matukio ya mafuriko katika Wilaya hizo ni zaidi ya miaka hamsini Sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here