Home KITAIFA MAJI YASIMAMISHA MWENGE WA UHURU ULANGA

MAJI YASIMAMISHA MWENGE WA UHURU ULANGA

Na Mwandishi wetu, Ulanga

MWENGE wa Uhuru Kitaifa 2024 uliokuwa tayari umewasili Wilayani Ulanga mkoani Morogoro Aprili 24 kwaajili ya kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali katika Wilaya hiyo umelazimika kusimama kwa zaidi ya saa moja baada ya maji ya mto Lulai uliopo kata ya Iragua kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wa wakazi wa kata ya Iragua wamesema kuwa wamekuwa wakisimamisha shughuli zao kwa zaidi ya masaa matano kutokana na mto huo kujaa maji pamoja na barabara inayounganisha Wilaya ya Ulanga na Malinyi kuwa korofi hivyo wanaiomba serikali iweze kuwatengenezea miundombinu ya barabara ili waweze kuendelea na shughuli za kijamii

“Tumeshukuru mwenge umekuja na umejionea changamoto ya hapa baada ya kusimama kwa zaidi ya saa moja lakini sisi huwa tunasimama zaidi ya saa tano shughuli za kijamii zinasimama tunaomba tutengenezewe barabara hii ili tuweze kusafirisha mazao yetu kwa urahisi kutoka eneo moja kwenda eneo jingine,“wananchi

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham amesema kuwa zaidi ya kaya 400 zimeathiriwa na maji pamoja hekta zaidi ya 5000 zimeenda na maji

“Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Jimbo langu la Ulanga zaidi ya kaya 400 zimeathiriwa na maji pamoja na kukosa makazi hivyo hali ni mbaya kwa wananchi wangu wanaenda kukumbwa na baa la njaa magari hayapiti na bidhaa zimepanda bei,“amesema Salim

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dk.Julius Ningu amesema kuwa kwa sasa bado wanasubiri maelekezo ya serikali juu ya changamoto hiyo ambayo bado inaendelea kuwatesa wakazi wa eneo hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here