Home KITAIFA *TAKUKURU PWANI  YAONGEZA MAPATO MACHINJIO MTAKUJA YA KIBAHA MKOANI PWANI

*TAKUKURU PWANI  YAONGEZA MAPATO MACHINJIO MTAKUJA YA KIBAHA MKOANI PWANI

Na Mwandishi wetu,  Pwani

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imefanya uchambuzi  wa mfumo  wa ukusanyaji  wa mapato yatokanayo na  machinjio ya Mtakuja iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha .

Akizingumza leo Aprili 24 Mkoani humo katika mkutano wake na waandishi wa habari Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani,  Ally Sadiki amesema taasisi hiyo imebaini    kuna uzembe  katika kusimamia idadi ya ng’ombe  wanao chinjwa  kwa siku husika na hakuna  ukaguzi kuhusu idadi ya ng’ombe  waliopo eneo la kusibiri kuchinjwa.

“Uchambuzi huu umefanywa  baada ya kupokea malalamiko  kutoka  kwa wananchi  kwamba  kuna miaya  ya rushwa  katika  ukusanyaji wa mapato  yatokanayo  na ushuru  katika machinjio hayo, hali  inayodababisha upotevu  wa mapato  na Halmashauri hiyo hivyo  kushindwa  kufikia  lengo la ukusanyaji  waliyojiwekea  kutoka  kwenye chanzo hiki,” amesema Sadiki.

Amesema uchambuzi  huo umebaini   kuwepo kwa mashine za kieletroniki za POS katika  machinjio kumekua  na taarifa  zinazokinzana ,kuwepo kwa tatizo la miundombinu na ucheleshaji wa kuweka fedha benki zinazo kisanywa.

“TAKUKURU  imebaini kuwa  idadi  ndogo  ya watumishi walioajiriwa  eneo husika ndiyo chanzo cha kushindwa  kutekeleza  majukumu ipasavyo,” aamesama.

Ameeleza kuwa  baada ya TAKUKURU  kuingilia kati makusanyo  yameongezeka  tofauti na ilivyokua  katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kati ya Oktoba na Desemba 2023 ambapo Oktoba  hadi Desemba  makusanyo  yalikua milioni 7,418,000 na sasa makusanyo  yameongezeka  na kufikia kiasi cha milioni 9,615,000.

“Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mji  ameongeza  watumishi eneo  hilo la machinjio ya Mtakuja kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi hivi sasa unafanyika  kila mara  ili kuondoa  fedha  za makusanyo  ya kila  siku na kuhakikisha  fedha  zinapelekwa benki kila siku,.

Sadiki amesema  kwa kipindi  tajwa  wamefanya chambuzi nyingine  za  mifumo  tano katika sekta  ya Ardhi, Elimu, AMCOS na ukusanyaji  na usimamizi wa mapato ya serikali ili kupata  tija  ya mifumo imara usiyokwamisha  utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza   kuwa TAKUKURU  Mkoa wa Pwani  wamefuatilia utekelezaji  wa miradi ya maendeleo 23 yenye thamani  ya biilioni 6.3 katika sekta za Elimu, Maji, Afya na Ujenzi (Barabara), ambapo kati ya miradi hiyo mradi mmoja umeonekana kuwa na upungufu  ufuatiliaji  unaendelea ii kurekebisha kasoro hizo. 

Pia Sadiki amesema kuwa katika kipindi hicho  cha miezi mitatu wameweza kutoa elimu kwa umma  kwa kufanya semina 19, mikutano yahadhara21,vipindi vya redio 9 kuimarisha klabu za wapinga rushwa 54 uandishi  makala 4 na TAKUKURU Rafiki6.

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Pwani imefungua  kesi mpya mbili Mahakamani ambapo kesi sita  zimeamuliwa  huku kesi nne watuhumiwa  wametiwa  hatiani na jumla kesi sita zinaendelea  Mahakamani. 

Amesema mikakati waliyojiwekea ni pamoja na  kuendelea  kufanya udhibiti wa mapato ya serikali na usimamizi wa rasilimali  za umma ikiwa  ni pamoja  na udhibiti wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here