Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA AWATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALIMBALI WAKATI SHAMRASHAMRA ZA MIAKA 60 YA...

RAIS DK.SAMIA AWATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALIMBALI WAKATI SHAMRASHAMRA ZA MIAKA 60 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Kuwatunuku Nishani Viongozi mbalimbali wakati wa shamrashamra za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili, 24 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MSamia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma Aprili, 24 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dk. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma Aprili, 24 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here