Na Mwandishi wetu,Dodoma
SERIKALI imesema imeanza uzalishaji wa umeme kupitia mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, ambapo uzalishaji huo umeanza kwa Megawati 235 kupitia mtambo namba tisa.
Hayo yamesema na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko Bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
“Matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba 2024 kwa mitambo yote nane yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 235 kila moja kuwa inazalisha umeme,”amesema Dk. Biteko