Home KITAIFA WAWEKEZAJI WAHAMASISHWA KUWEKEZA TANGA

WAWEKEZAJI WAHAMASISHWA KUWEKEZA TANGA

Mkoa wa Tanga umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini

Wafanya biashara waaswa kuzingatia Sheria za Madini

Na Mwandishi wetu, Tanga

AFISA Madini, Winnifrida Mrema ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini mkoani Tanga kutokana na uwepo wa aina mbalimbali za rasilimali madini mkoani humo.

Wito huo umetolewa leo Aprili 23, 2024 jijini Tanga na Mrema wakati akizungumza na Waandishi wa Habari amesema, Mkoa huo umebarikiwa kuwa na aina mbalimbali za madini yakiwemo Madini ya metali kama vile madini ya Dhahabu, Chuma na Shaba, Madini ya Viwandani kama Kinywe, Bauxite, Chuma, Jasi, Chokaa, Ulanga, Dolomite, Feldspar, na Chumvi, na MadinI Ujenzi.

Amesema mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini ya vito hapa nchini ambapo ametaja aina mbalimbali ya vito vinavyopatikan mkoani humo ikiwa ni pamoja na Garnets za aina mbalimbali, Rubi, Tourmaline za aina mbalimbali, Sapphire, na Zircon na Tangastone.

Pia, Mrema amesema madini mengine yaliyopo mkoani humo ni pamoja na Madini Tembo (Heavy mineral sand), Bauxite, Chumvi, Ulanga (Mica), na Quartz

“Mkoa huu umejaliwa kuwa na viwanda vikubwa vinne vinavyotumia madini mbalimbali kwa ajili ya kuzalisha wa saruji na chokaa. Viwanda hivyo ni pamoja Tanga Cement, Maweni na Kilimanjaro vinavyozalisha saruji, pamoja na kiwanda cha chokaa cha Neelkanth,”amesema Mrema.

Amesema Dunia inauhitaji mkubwa wa madini mkakati hivyo ametoa wito kwa wawekezaji wakubwa na wadogo kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika madini mkakati ya Kinywe na Madini Tembo ili kujipatia faida na kunufaisha mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewasisitiza Wamiliki wa Leseni za Uchimbaji wa Madini na wafanya biashara wa madini kuzingatia Sheria na Kanuni za Madini hususan kwa wafanya biashara ya madini ya dhahabu na vito kufanya biashara zao kupitia masoko ya madini.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Uthaminishaji wa Madini ya Vito, Visetasi Kiding’a amesema, hadi sasa mkoa wa Tanga bado hauna wawekezaji wa kutosha kulinganisha na fursa za shughuli za madini zilizopo mkoani humo ambapo ametoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kwa ajili ya kuomba leseni za uchimbaji na ufanyaji biashara ya madini mkoani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here