-Awatoa hofu wananchi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
Na Mwandishi wetu@Lajiji Digital
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo April 23, 2024 ametembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara hiyo Chalamila amekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo daraja la kibada ambapo TANROAD wanaendelea na matengenezo ya daraja hilo ili kurejesha mawasiliano.
“Niwatoa hofu wananchi kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ambapo Dar es Salaam ni salama hakuna barabara ambayo itaachwa bila kutengenezwa barabara zote zitatengenezwa katika viwango tofauti,wananchi waendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kuhama mabondeni,” amesema Chalamila.
Vilevile ameelekeza kuanza kwa oparesheni ya kuondoa vipenyo ili kuruhusu maji yapite ikiwemo kubomoa Kuta zinazuia maji kupita.
Chalamila amezitaka Halmashauri zote katika Mkoa huo kutoa fedha ambazo ziliwekwa katika bajeti kwa ajili ya TARURA ili Kuharakisha urekebishaji wa maeneo yote yaliyoharibiwa na mvua
Mwisho RC Chalamila amezitaka TANROAD na TARURA kufanya kazi usiku na mchana katika nyakati hizi za mvua Kabla ya usiku wa kesho April 24, 2024 barabara ziwe zinapitika.